Friday, 25 March 2016

Johan Cruyff amepoteza maisha kwa kansa leo, Rais Kikwete na Shein watamkumbuka kwa hili.

Ulimwengu wa soka March 24 2016 umepata taarifa za msiba wa nguli wa soka wa Uholanzi aliyewahi kuvichezea vilabu vya Ajax na FC Barcelona ya Hispania Johan Cruyff. Nguli huyo ameripotiwa na BBC Sport kufariki kwa kansa leo akiwa na umri wa mika 68.


D92A5259
Johan Cruyff pia aliwahi kuja Tanzania na kumpatia zawadi ya jezi rais mstaafu wa awamu ya nne DK Jakaya Kikwete
Kama utakuwa unakumbukumbu nzuri, Johan Cruyff ndio staa wa Uholanzi aliyeliongoza taifa hilo katika fainali ya Kombe la Dunia 1974 na kupoteza mechi hiyo dhidi ya Ujerumani Magharibi. Rais Shein wa Zanzibar na Rais mstaafu Jakaya Kikwete wamewahi kukutana na nguli huyo na kupewa zawadi ya jezi.
_88252809_cruyff_barcasupport_getty

Wachezaji wa FC Barcelona waliwahi kuvaa t-shirt zenye ujumbe wa kumtakia kheri nguli huyo miezi kadhaa nyuma.
Johan Cruyff amefanikiwa kutwaa mataji kadhaa, ikiwemo tuzo ya Ballon d’Or mara tatu, ameshinda Kombe la Ulaya mara tatu akiwa na Ajax, lakini ameshinda taji hilo pia mwaka 1992 akiwa na FC Barcelona. Cruyff anatajwa na atakumbukwa kama mmoja kati ya wachezaji bora wa muda wote, kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

IMG_0396
Hapa alikuwa akimkabidhi zawadi ya jezi Rais Shein wa Zanzibar.

No comments: