Monday, 14 March 2016

FIFA yaadhibu wakuu wa soka Afrika Kusini

Image copyrightAFP
Image captionFIFA yaadhibu wakuu wa soka Afrika Kusini
Shirikisho la soka duniani FIFA limewapiga marufuku
maafisa 3 wa shirikisho la soka la Afrika Kusini kwa tuhuma za kupanga mechi.
Maafisa hao watatu wakiongozwa na aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Leslie Sedibe amepigwa marufuku ya miaka 5 na kupigwa faini ya dola elfu $20,245 .
Maafisa wengine waliopigwa marufuku ni Steve Goddard na Adeel Carelse, ambao waliwahi kuwa viongozi wa idara ya waamuzi katika SAFA.
Wawili hao wamepigwa marufuku ya miaka miwili kila mmoja.
Kauli hiyo imeafikiwa baada ya uchunguzi wa kina ulioendeshwa na FIFA uliobaini kuwa mechi za kirafiki kabla ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 zilipangwa.
Image copyrightAFP
Image captionWawili hao wamepigwa marufuku ya miaka miwili kila mmoja.
Tayari kiongozi mmoja wa magenge ya kupanga mechi raia wa Singapore bwana Wilson Raj Perumal amehukumiwa kifungo kwa makosa hayo

No comments: