Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Mjini kwa ruhusa ya chama cha ACT Wazalendo, na kwa siku kadhaa amekua akihusishwa na headlines za kutokuwa na uhusiano mzuri yeye na Mwenyekiti wa chama chake cha zamani cha CHADEMA Freeman Mbowe ila leo February 3’amezichukua headlines kwa kuandika yafuatayo.
>>>> ‘Chama chochote makini huweka tofauti binafsi pembeni Kwa maslahi mapana ya Taifa. Chama cha ACTwazalendo kinaamini katika umoja, mimi, nikiwa Mbunge waACTwazalendo natekeleza Kwa vitendo maelekezo ya chama Kwa kushirikiana na wabunge wenzangu wa upinzani bungeni’
Nafasi ya ACTwazalendo Bungeni ni upande wa upinzani na hivyo tutakuwa na wenzetu katika upinzani kwenye hoja zote za kitaifa, tunaweza kupishana kwenye mkakati wa utekelezaji, hatuwezi kupishana kwenye maslahi ya Nchi yetu ya kujenga demokrasia na kukataa udikteta.
>>> ‘Mimi binafsi siwezi kuwa mfungwa wa magomvi yetu ya miaka ya nyuma, nilishasamehe walionikosea na kuomba radhi niliowakosea #ForwardEver, Mbowe siku zote amekuwa kiongozi wangu na siwezi kubeza nafasi yake katika kujenga demokrasia nchini. Tulipishana. Tulikoseana. Tusameheane‘
>>> ‘Kwangu mimi huu ni wakati muhimu sana kuwa na United Front ya upinzani ndani ya Bunge ili kuzuia udikteta unaonyemelea nchi yetu’
Zitto Kabwe ameyaandika haya na kuambatanisha na post yake kwenye mtandao wa Instagram akinukuu gazeti la Mwananchi lilimnukuu Freeman Mbowe akisema yafuatayo >>> ‘”Kushirikiana na Zitto si jambo la ajabu kama ambavyo umeona tukifanya. Yapo majeraha mengi ambayo tumeyapitia pande zote (Chadema na Zitto) ambayo huwezi kuyatibu kwa siku moja, yapo ambayo yatapona kulingana na muda,unaweza kumfanyia mtu kitu kibaya lakini baadaye ukatambua kuwa umekosea chochote katika siasa kinawezekana.
No comments:
Post a Comment