Monday, 14 March 2016

Kesi dhidi ya ushindi wa Museveni yaanza kushika vuguvugu huko uganda.

Image captio
Kesi inayopinga matokeo ya uchaguzi
mkuu wa urais nchini Uganda uliofanyika Feb 18 mwaka huu imeanza rasmi mjini Kampala.
Mtuhumiwa wa kwanza kwa wale walioshtakiwa amefika kizimbani.
Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango anasema kuwa Majaji nchini Uganda wameanza kusikiza kesi ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi jana.
Mmoja wa mashahidi muhimu, Dr Badru Kigunddu, mkuu wa tume ya uchaguzi ndie ametangulia kizimbani na alipoulizwa na mawakili wa mlalamishi wakati fulani aliomba msamaha kwa wapiga kura wa mjini Kampala pamoja na wilaya jirani ya Wakiso ambako inasemekana ni ngome za upinzani ambako vifaa vya kupigia kura vilichelewa kufika maeneo hayo.
Tume ya uchaguzi ilimtangaza Museveni kama mshindi wa asili mia 61% na upinzani kupinga ushindi huo wakisema ulikumbwa na udanganyifu.
Hata hivyo kikao cha jioni kiliahirishwa mapema na jaji Bart Katureeebe baada ya nyaraka fulani kukosekana mahakamani
Image captionAliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi ndiye aliyewasilisha kesi hiyo mahakamani
Jaji ameahirisha kikao hadi kesho.
Kesi ya kupinga matokeo hayo imefikishwa mahakamani na mtu aliyechukua nafasi ya tatu katika uchaguzi huo ulioandaliwa na tume ya uchaguzi na aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi.
Mshindi wa pili kanali mstaafu Kizza Besigye hakuweza kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo kwani anatumikia kifungo cha nyumbani.
Majaji wa mahakama hiyo ya kilelecha wapatao tisa wanapaswa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi huu

No comments: