Kosa la kupoteza mchezo wowote kwa
Borussia au Bayern Munich itakua advantage kubwa kwa timu moja wapo kati
ya hizi mbili. Hadi sasa hivi kuna tofauti kati ya point 5 kati yao na
wote wana uwezo wa kuchukua ubingwa kutokana kuwa na vikosi imara vyenye
wafungaji wakali.
Kwenye mechi dhidi ya Wender Bremen,
Aubamenyang alifunga goli la kwanza dakika ya 53 na kuwapa nafasi ya
kuongoza mechi hiyo. Dakika ya 60 Wender Bremen walirudisha goli na
kuongeza dakika ya 75.
Kama mchezo ungeisha hivyo Borussia
wangekua na tofauti ya point 8 na Bayern Munich lakini magoli ya Shinji
Kagawa na Adrian Ramos yaliwapa point 3 muhimu.
Hadi sasa club zote mbili zimeshacheza
mechi 28 wakati Bayern wakiongoza kwa points 72 wakifuatiwa na Borussia
wenyee points 67. Mechi zote za Bundesliga zinaonekana Live kwenye
Startimes.
|
No comments:
Post a Comment