Sunday, 3 April 2016

Nnauye ashiriki kutazama mechi ya mbeya city na costoal union..

N1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa (kushoto) alipowasili katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kuangalia mchezo kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya.
Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi makalla
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi kabla ya kuanza mechi yao na Mbeya City jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.
N3
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Coastal Union na Mbeya City wakisakata kabumbu jana Jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilitoka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.
N4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifuatilia kwa makini mchezo wa mpira wa miguu kati ya Mbeya City na Coastal Union ya Tanga jana Jijini Mbeya baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini hapo. Kushoto kwa Mhe.  Nnauye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla na wakwanza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg. Halhaji Kundya.
   
N5
Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia ushindi wa timu yao ya Mbeya City baada ya kuichapa timu ya Coastal Union ya Tanga mabao manne kwa sifuri jana katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.


No comments: