Sunday, 3 April 2016

Real madrid yaigalagaza barcelona usiku wa jana.


Wakati makocha hawa walipokuwa wachezaji, walikuwa mastaa wakubwa katika vilabu vyao vya Barca na Real, na sasa ndio wanaviongeza vikosi vya timu hizi wakiwa kwenye mabenchi. – Luis Enrique akiwa kwenye msimu wake wa pili na FC Barcelona na tayari ameshashinda makombe matano na ameshaiongoza Barca kwenye Clasico tatu – akishinda 3-1 Bernabeu na 2-1 Nouc Camp, wakati wa msimu wake wa kwanza dhidi ya Ancelotti na msimu huu ameshinda 4-0 @Bernabeu dhidi Rafa Benitez.
 Zidane amekuwa kocha wa Madrid kuanzi January 4, 2016, akimbadili Rafa Benitez. Mpaka sasa ameiongoza Madrid kushinda mechi 9 za La Liga, sare 2 na akipoteza moja. Luis Enrique alikuwa akiitumikia Barca kama mchezaji kuanzia 1996 mpaka 2004, wakati Zidane alivaa jezi za Madrid kuanzia 2001 mpaka 2006. Wamewahi kukutana katika mechi 7 za El Clasico – Zidane akifunga magoli mawili katika msimu wake wa kwanza  – yote katika uwanja wa Nou Camp – sare ya 1-1 katika ligi na ushindi wa 2-0 katika Champions League.

Luis Enrique pia amewahi kuifunga Madrid wakati Zidane akiwa Los Blancos, goli la kusawazisha katika sare ya 1-1 pale Santiago Bernabeu msimu wa 2002/03 season.
Je leo nani ataibuka kidedea – muda mfupo ujao tutapata majibu
 

No comments: