Jeshi
ni sehemu muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga
bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani
huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha
na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki
idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo
na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao
wa kiusalama.
Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake.
Japan
ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia (WW2)
iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo, Japan
iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la kawaida
lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua tena
jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake.
Bajeti ya Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 49.
Jeshi
hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000 waliopo kazini na zaidi 60,000 wa
akiba. Lina ndege za kivita zipatazo 1,595 na meli 131.
|
No comments:
Post a Comment