Afrika ni bara ambalo tafiti kadhaa zinafanyika na zimeendelea kufanyika, Matokeo ya Utafiti wa Africa Wealth umeitaja Zimbabwe kuwa ndio nchi Maskini. Inatajwa
kuwa wizi wa kura, ukosefu wa kuheshimu haki za umiliki, vurugu,
kukosekana kwa uhuru wa Habari, ni baadhi ya sababu ya Taifa hilo
kuanguka na kuwa la mwisho.
Ripoti ya
tatu ya mwaka ya Africa Wealth inasema watu wanaoishi Zimbabwe ni
maskini katika bara la Afrika kwa kuwa na wastani wa pato la mtu
mmojammoja ni US dola 200 ambapo ni kiasi ambacho watumishi wa umma
wanakipata.
Ripoti imeeleza kuwa >>>’haki
za umiliki ni muhimu kwa kuwezesha kujenga utajiri, Nchini Zimbabwe
wamiliki wa Biashara hawana uhakika kama biashara zao au mali zao bado
ni zao, hii inajenga hali ya woga kwa yeyote kutojitokeza kuwekeza
kwenye nchi hiyo‘
Wakati
Zimbabwe ikianguka na kuwa nchi maskini, kisiwa cha Maurtius kimepanda
na kuonekana kuwa watu wake ni matajiri kwa hadi pato la US dola 21700
kwa utajiri wa mtu mmojammoja. Mafanikio ya Mauritius yamehusishwa na
kupata haki za umiliki ambapo imeshuhudiwa watu matajiri wakihamia huko
katika muongo uliopita.
Utafiti uliofanyika kwenye nchi 20, zote zimekuwa na ongezeko la pato kwa kipindi cha mwaka 2000 na 2015, kasoro Zimbabwe
No comments:
Post a Comment