Thursday, 17 March 2016

Picha: Kubadili dhana ya Afrika kupitia sanaa

 Picha: Kubadili dhana ya Afrika kupitia sanaa

Maonyesho ya sanaa katika makavazi ya Guggenheim mjini Bilbao, kaskazini mwa Uhispania, inalenga kuonyesha kizazi kipya cha Waafrika ambao wanalipa bara hili mtazamo mpya. Maonyesho hayo kwa jina Making Africa yanashirikisha wasanii 120.
Mmoja wa wale ambao kazi zao zinaonyeshwa ni mpiga picha kutoka Senegal Omar Victor Diop. Kazi zake huangazia kuonyesha mchanganyiko wa tamaduni nyingi nchini humo. Hufanya kazi na wahusika, kama huyu Mame-Diarra Niang kwenye picha ambayo Diop aliipiga kuonyesha sifa mbalimbali za watu.Mpiga picha kutoka Msumbiji Mario Macilau hulenga kuonyesha
kizazi kipya cha vijana mji mkuu Maputo. Kando na kuonyesha usasa, picha zake pia hujaribu kuonyesha studio zilivyokuwa zamani. 
Mkenya Cyrus Kabiru naye hutengeneza vitu mbalimbali kutoka kwa vitu vilivyotupwa kama taka. Ametengeneza vitu vingi sana vya kuvaliwa, kwa mfano miwani hii, ambayo inadhamiria kuonyesha jinsi Afrika kutazamwa visivyo.
Bodys Isek Kingelez naye dhamira yake kuu ilikuwa kuonyesha majengo ya siku za usoni na kukosoa mtazamo wa miji ya Kimagharibi.
Muundo huu wake, aliouita Congolese Red Star, pia unaashiria maadili ya kijamaa na msanii huyu anasema anataka kuunga ulimwengu wenye miji iliyojaa "amani, haki na uhuru". 
Raia wa Nigeria JD Okhai Ojeikere naye ameangazia jinsi wanawake husuka nywele zao. Alitaka kuweka kumbukumbu ya mitindo yote ya kusuka nywele pamoja na kuwafanya watu wengi zaidi kuikumbatia.Pierre-Christophe Gam ndiye aliyeunda tovuti ya mwanamuziki Taali M. Alitaka kutumia tovuti hiyo kumsafirisha mtazamaji hadi ufalme wa kale wa Afrika kwa kutumia mwanamuziki huyo Mfaransa, ambaye ana asili ya Congo, Chad na Misri.Mkenya Wangechi Mutu kwenye filamu yake fupi kwa jina The End of Eating Everything (Mwisho wa Kula Kila Kitu) anakosoa jamii yenye kuangazia sana matumizi. Filamu hiyo inamuonyesha mhusika mmoja akila nzige na mwishowe analipuka na kutokwa na vichwa vingi.
Picha za Malick Sidibe zilizopigwa nchini Mali miaka ya 1960 nazo zinaakisi hisia za uhuru zilizokuwepo wakati huo, na ambazo wasanii wa kisasa wanajaribu kurejesha. Picha hii ya 1963 inaonyesha vijana wawili wakifurahia kujumuika pamojaMchoraji mijengo David Adjaye aliombwa kutayarisha mchoro wa kibanda kipya kwenye kituo cha uchukuzi jiji la Johannesburg, Afrika Kusini. Mchoro wake unatoa hisia za usasa na kale
. 
Maonyesho hayo ya sanaa ambayo kwa Kiingereza yanaitwa Making Africa yataendelea mjini Bilbao hadi Februari 21.

No comments: