Zaidi ya nyumba 50 ikiwemo ya mkuu wa jeshi la polisi mstaafu katika
manispaa ya moshi mkoani Kilimanjaro zipo hatarini kubomolewa wakati
wowote baada ya kujengwa kinyume cha sheria ya mipango miji na sheria ya
hifadhi ya mazingira ambayo ni kando ya mto Karanga.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Bw.Novatus Makunga amesema hayo baada ya kukagua
baadhi ya nyumba akiwa na kamati ya ulinzi na usalama na kujiridhisha
juu ya ujenzi wa nyumba hizo kinyume cha sheria..
Bw.Makunga ambaye ameipa siku saba manispaa hiyo kutoa taarifa rasmi
juu ya ujenzi holela amesema,serikali inafanya uchunguzi wa kuwabaini
baadhi ya maafisa ardhi wa manispaa hiyo waliotoa vibali vya ujenzi wa
nyumba hizo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw.Danford Kamenya amesema, kamati
hiyo pia imeyatembelea baadhi ya maeneo ambayo wafanyabiashara
ndogondogo wamepanga bidhaa zao chini na kuangalia namna ya kuwatafuia
maeneo mengine ya biashara.
No comments:
Post a Comment