Wakati
polisi wakikimbizana na makahaba wanaojiuza katika maeneo mbalimbali
maarufu na klabu za usiku, biashara hii sasa imehamia katika mitandao ya
kijamii.
Biashara
hiyo ambayo awali ilikuwa ikifanyika katika viambaza vyenye mwanga
hafifu katika maeneo maarufu, sasa inafanyika kwa uwazi katika mitandao.
Gloria,
mmoja wa wanawake ambao kwa zaidi ya miaka 20 amefanya biashara hiyo
anasema: “Biashara imebadilika sana, huhitaji kutumia nguvu nyingi au
kutangatanga kupata mteja... unaingia tu mtandaoni wamejaa tele.”
Mwanamke huyu anasifu ukuaji wa teknolojia akisema umeisaidia biashara
hiyo kwani pamoja na kuirahisisha, pia umeipa thamani kwa kuwa bei ya
mtaani na mtandaoni ni tofauti kabisa.
Jinsi inavyofanyika
Kwa
mujibu wa Annie Jameson (siyo jina lake halisi) biashara hii hufanyika
kupitia tovuti mbalimbali (dating sites), mitandao ya kijamii kama
badoo, facebook, wechat na ile ya simu za mkononi BBM, WhatsApp na
telegram.
Anasema
watumiaji hutofautiana kutokana maeneo walipo, akitolea mfano hapa
nchini alisema: “Bado wanunuzi na wauzaji hawatumii dating sites kwa
sababu utaingia kwenye matatizo na Serikali. Wenzetu wamefikia hatua
hiyo lakini hapa mitandao tunayotumia ni ile inayopunguza wigo wa
taarifa kusambaa kwa uwazi,” anasema.
Alisema
ingawa biashara hiyo imeshamiri nchini lakini inafanyika kwa ustadi ili
wasiharibu soko hasa kwa wanaume ambao ndiyo wateja wao.
“Unajua
wanaume wanapenda sana hivi vitu lakini wanataka kulinda heshima zao,
kwa hiyo ukijiweka kwenye dating sites inakuwa ngumu kidogo kukufuata,
lakini kwenye WhatsApp au BBM ‘fastaa’ wanakuja,” alisema. Biashara hiyo
kupitia WhatsApp imechukua kasi zaidi kutokana na kuwapo kwa mtu wa
kati (supplier) ambaye anakuwa na wasichana zaidi ya 20 ambao anakuwa na
picha zao kwa ajili ya wateja wanaowahitaji.
Kwa kutumia mtandao huo, mteja anapotaka msichana huomba kwa ‘supplier’ atumiwe picha ili achague anayemtaka.
“Ni
rahisi siku hizi wala huhangaiki kama una hela unapata picha unachagua
halafu unaeleza ulipo anakuja kwa gharama ya kuanzia Sh20,000 mpaka
Sh100, 000 inategemea tu kiwango cha msichana mwenyewe na nguvu yako
katika kuomba punguzo,” alisema mmoja wa wateja na kuongeza:
“Masupplier wapo kibao siku hizi hata ukiwa mkoani unaweza kuwasiliana na ambaye unamjua Dar es Salaam unashushiwa tu kazi.”
Mteja
mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema alikuwa hajui
anawezaje akapata wanawake wanaojiuza kwa njia hiyo hadi alipoelezwa na
marafiki zake mtaani.
“Palepale
akanionyesha na kuniunganisha na mwenye mademu kisha nikamrushia
supplier Sh10,000 halafu nikaletewa picha zaidi ya 10 nikachagua na
kuelekeza nilipo, demu akaja na pikipiki hadi pale tulipokuwa kazi ikawa
imeisha.”
Alisema
gharama ya huyo msichana mwenyewe ilikuwa ni Sh100,000 lakini akitaka
apate kinywaji au chochote gharama zitakuwa juu ya mteja.
“Gharama nyingine ni zako mwenyewe anakuja kwa shughuli moja tu,” alisema.
Kinachoendelea mitandao mingine
“Naitwa
Baker, nahitaji jimama kama wewe wa kunilea mimi nitakupa mapenzi hadi
uchoke, namba zangu hizo 071......(anaziandika). Hivyo ndiyo ulivyoanza
ujumbe katika mtandao wa marafiki wa Badoo. Mbali ya mtandao huo,
mabinti wengi, hasa wa vyuo wameanzisha akaunti katika mitandao
mbalimbali ikiwamo Facebook, Twitter, Instagram, Imo na mingine mingi
kwa ajili ya kunadi biashara ya ngono.
Mitandao
mingine inayotumika katika biashara hiyo ni Tinder, Lovoo, SpeedDate,
BeNaughty, Are You Interested na SayHi. Mitandao hii si tu huwakutanisha
wanawake hao na wanaume wa ndani, bali hata wa nje ya nchi hasa kwa
wale wanaotafuta Wazungu.
Msichana
mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema amesafiri kwenda nchi
mbalimbali zikiwamo Kenya, Ghana na Marekani kwa shughuli za ngono baada
ya kukutana na wanaume kwenye mitandao hiyo na kukubaliana.
Alisema
amewahi kuwakutanisha rafiki zake zaidi ya 10 katika mitandao na
kuangalia umbali wa wanaume wanaozungumza nao na kuoanisha na maelezo.
“Kuna
mitandao, ukiwamo SayHi!, inakupa hadi ramani huyo mtu alipo. Hii
inakusaidia kujua taarifa za mteja unayechati naye kwa kuwa wengine huwa
waongo,” alisema.
Msichana
huyo alisema mbali na kwenda nchi za nje, hapa Tanzania amekwenda
katika mikoa mingi kufuata wateja wa ngono, Zanzibar ikiongoza.
Mmoja
wa wanaume wanaotumia mitandao kusaka ngono, alisema: “Nilikutana binti
mtandaoni, nikamfuatilia, tukakutana naye maeneo ya Duce (Chang’ombe,
Dar es Salaam), tukaenda Keko, nimekuwa naye hadi asubuhi hii, nimempa
Sh50,000 kama tulivyokubaliana.
“Alitaka
150,000 na alivyovaa, ningekuwa nayo ningetoa nilivyomwambia sina
tupange siku nyingine akaniuliza nina ngapi nilipomwambia nina Sh50,000
tu aliniambia lete hiyohiyo kwa leo,” alisema kijana huyo.
Kijana
mwingine, Abdulrazaq Ibrahimu amewahi kukutana na wasichana wengi
mtandaoni lakini tofauti na wengine, alikuwa akifanya utafiti akitaka
kufahamu jinsi biashara ya ngono inavyohusisha watu wa hadhi, vyeo, umri
na madaraja tofauti.
Alisema
kati ya wasichana wasiopungua 25 aliokutana nao mtandaoni, hakuna
aliyemkawiza eneo la miadi kwa muda mrefu. Wapo aliowakuta wamefika na
wengine wakifika baada tu ya kuwaambia amefika eneo husika
No comments:
Post a Comment