Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ain ambaye analipwa kiasi cha $200,000
kwa wiki amenunua jumba hilo lenye thamani inayokadiriwa kufikia dola
millioni 3 za kimarekani ambazo zinafikia billioni 6 za kitanzania.
Jumba hilo lipo maeneo ya McCarthy Hills enclave jijini Accra lina
baa mbili, bwawa kubwa la kuogelea. Lina ghorofa tatu zilizotengenezwa
kwa muundo wa kipekee kila mmoja huku vifaa vya ulinzi vikiwa vya kisasa
ikiwepo milango na madirisha yenye bullet proof.
Kwa mujibu taarifa za vyombo vya habari vya Ghana, Gyan aliinunua
nyumba hiyo aliyoikarabati alipozuru nchini humo mwezi April wakati
alipoenda kutazama pambano la masumbwi kati Emmanuel Tagoe na Jobert
Delos Reyes.
No comments:
Post a Comment