Kitu muhimu katika maisha ya wanasoka wakubwa duniani sio tu kupata na kulipwa mshahara mkubwa, bali mataji ni miongoni mwa vitu ambavyo wachezaji wanavipa kipaumbele, March 2 nimekutana na list ya majina ya wachezaji sita mahiri kutokasokka.com waliowahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia, lakini wameshindwa kutwaa taji la UEFA.
6- Michael Owen ni mchezaji wa mwisho wa Uingereza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mwaka 2001, jamaa amewahi kushinda mataji kadhaa, lakini ameshindwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kuwa na mafanikio.
5- Pavel Nedved ni moja kati ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia akiwa na umri wa miaka 19 na klabu yake ya Lazio, Pavel pia anatajwa kama mchezaji mwenye mafanikio kutokea Czezh, lakini hakuwahi kutwaa taji la UEFA.
4- Fabio Cannavaro ni beki wa kati wa Italia na amewahi kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na timu yake ya taifa ya Italia, licha ya kuwa alitamba na vilabu vyaJuventus, Real Madrid na Inter Milan hakufanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
3- Lothar Matthaus aliiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1990, mwana unaofuatia Lothar aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ujerumani kutwaa tuzo ya Ballon d’Or na ndio mchezaji pekee wa Ujerumani kuwahi kutwaa tuzo hiyo.
2- Ronaldo ametamba na vilabu vingi kwa mafanikio barani ikiwemo FC Barcelona naInter Milan, Ronaldo amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara tatu pamoja na Kombe la Dunia lakini hakuwahi kutwaa taji la UEFA.
1- Robert Baggio huyu huwa anapewa heshima ya kama mmoja kati ya wachezaji bowa wa muda wote kuwahi kutokea, amewahi kutwaa mataji mawili ya Ligi, Copa Italia pamoja na UEFA lakini hakuwa sehemu ya timu iliyosaidia kutwaa taji hilo.
No comments:
Post a Comment