Uchaguzi mkuu kwenye nchi ya Uganda umefanyika leo kwa watu kupiga kura ya nani wanamtaka awe Rais wao ambapo upinzani mkubwa kwa Rais Museveni aliyeiongoza Uganda kama Raisi kwa miaka 30 unatokea kwa Kizza Besigye.
Mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Whatsapp ilifungwa na serikali ya Uganda kwenye siku hii ya uchaguzi pamoja na huduma za kutuma na kupokea pesa kupitia simu za mkononi kwa kile kilichoelezwa kwamba ni ombi la baraza linalosimamia uchaguzi kuzuia pamoja na ishu nyingine, uenezwaji wa habari za uongo.
Mtandao wa simu wenye watumiaji zaidi ya milioni 10 MTN uliamrishwa kuzima mitambo yake kutii agizo lililotolewa la kukata mawasiliano hayo (kwa mujibu wa BBC) ambapo Rais Museven alipohojiwa na vyombo vya habari alisema dhumuni la hatua hiyo kuchukuliwa ni kuepusha ueneaji wa habari za upotoshaji kama anavyoongea kwenye hii video hapa chini.
Museveni: Blocking of social media sites and MM services done in the interest of national security #UgandaDecidespic.twitter.com/2NEA4N4Xvh— NBS Television (@nbstv) February 18, 2016
Wakati huohuo Mgombea Urais mwenye ushawishi mkubwa wa nchi hiyo Kizza Besigye alikamatwa tena leo na Polisi nje ya nyumba ambayo upinzani unasema wizi wa kura ulikua ukifanyika, ripoti ya usiku wa February 18 2016 ni kwamba Besigye ameachiwa huru… tazama hii video hapa chini.
No comments:
Post a Comment