Waandishi wa habari waaswa
kujiendeleza kielimu katika fani ya uandishi wa habari na taaluma
nyingine ili waweze kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili jamii.
Wito huo umetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria Dr. Hamza Kondo alipokuwa
akizindua kitabu chake kiitwacho Watchdog Journalism in Tanzania a
Sustainable Struggle ambapo kwa Kiswahili ni “Uandishi Habari Huru
Tanzania ni mapambano endelevu”.
Dr Kondo amesema lengo la kitabu
hicho ni kuwaelimisha na kuwaasa waandishi wa habari na wataaluma ya
habari kuzidi kuithamini taaluma hiyo licha ya changamoto
zinazowakabili.
Amesema kitabu hicho
kinazungumzia uhalisia wa uhuru wa habari nchini, hivyo kinafaa
kufundishia taaluma ya habari katika vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini.
Aidha, Mhadhiri huyo ameongeza
kuwa ili fani ya taaluma ya habari iheshimike ni lazima iwe na bodi ya
wataalamu waliobobea ambayo itaundwa na wasomi wa taaluma husika ili
kusimamia maadili ya taaluma hiyo na kuchukua hatua kwa wanataaluma
watakaokiuka maadili.
Mbali na hayo Dr Kondo ametoa
zawadi ya vitabu kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini likiwemo gazeti
la Jamuhuri, gazeti la majira, gazeti la Habari Leo, gazeti la Mwananchi
na gazeti la Nipashe.
No comments:
Post a Comment