Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akizungumza na wadau (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la uwajibikaji katika sekta ya
Mafuta na Gesi lililoandaliwa na taasisi ya WAJIBU – Institute of Public
Accountability leo Aprili 11,2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick
Utouh akizungumza na wadau waliyoshiriki Kongamano linalohusu
uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi (hawapo pichani) kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango (kulia) akikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public
Accountability na (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
Bw.Ludovick Utouh,sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau waliyoshiriki Kongamano linahusu Uwajibikaji katika sekta ya
Gesi na Mafuta wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi
wa Taasisi ya TWAWEZA Bw.Aidan Eyakuze (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick
Utouh wakiwa wanaonesha kibao kinacho onyesha ufunguzi rasmi wa taasisi
hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (wanne kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliyoshiriki Kongamano la Uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi,(watatu kulia ni)aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na (watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh
No comments:
Post a Comment