Staa wa muziki
nchini Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz ametakiwa kutoka Jijini
Dar es salaam na kurejea Mkoani Kigoma alikozaliwa, ili kuwasaidia
Wasanii chipukizi katika Mkoa huo.
Mbali na Diamond,
Staa mwingine alietajwa ili atoke Jijini Dar es salaam na Kurejea Mkoani
kwake ni Farid Kubanda a.k.a Fid Q, ambae ametakiwa kurejea Jijini
Mwanza ili kusaidia kuukuza muziki wa Mwanza.
Mbali hao mastaa
hao ambao wametajwa live majina yao, pia mastaa wote waliohamishia
shughuli zao za sanaa Jijini Dar es salaam wametakiwa kurejea katika
Mikoa yao ili kuondoa mrundikano wa wasanii katika Jiji hilo.
Hayo yalisemwa
juzi ijumaa Jijini Mwanza na Msanii Chipukizi Joseph Stanford a.k.a
Rich4D, katika hafla ya kumpongeza kwa ushujaa wake wa kutembea kwa
miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya
Kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wa wasanii
nchini na kuwajumuisha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo.
"Wasanii wakubwa
watoke Jijini Dar na warudi Mikoani kwao ili wawasaidie wasanii
chipukizi wa Mikoani. Diamond arudi Kigoma. Fid Q arudi Mwanza. Hii
itaondoa mrundikano wa wasanii wakubwa Dar na hivyo kupeleka fursa za
sanaa mikoani". Alisema Rich4D.
Matembezi ya Miguu
ya Msanii Rich4D yalianza Januari 16,2016 yakihusisha mikoa minane sawa
na Kilomita 1,200 na yalifikia tamati Februari 10,2016, lakini adhma
yake ya kuonana na rais haikuweza kutimia baada ya rais kuwa katika
majukumu mengine ya kitaifa ambapo aliekuwa Katibu Mkuu Ombeni Sefue
aliahidi msanii huyo kuonana na rais.
Wadau mbalimbali
waliosaidia kufanikisha matembezi hayo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Nyamagana Raphael Shilatu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana
Stanslaus Mabula, wameyapongeza matembezi hayo na kusema kuwa ni ya
kizalendo ambapo wamemuomba Katibu Mkuu Mpya, Mhandisi John Kijazi
kuhakikisha ahadi aliyoiacha Sefue inatimia ili msanii Rich4D afanikiwe
kuonana na rais magufuli.
Staa Fid Q
Msanii Rich4D anaechipukia kwa kasi Jijini Mwanza ambapo tayari anatamba na ngoma mbili ambazo ni "Tawile" na "Huniwezi".
No comments:
Post a Comment