Waziri
Mkuu, Kassim Majalaiwa akizungumza na Madaktari, Wauguzi na watumishi
wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa Aprili 11, 2016. Kushoto ni Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa
Lindi, Mzee Mtopa.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majalaiwa akizungumza baada ya kukabidhi msaada
wa shuka kwa wazazi wanaosubiri kujifungua na waliojifungua kwenye
hospitali ya wilaya ya Ruangwa Aprili 11, 2016. Kushoto ni Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa
Lindi, Mzee Mtopa.
Wanawake
wa Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti
alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu mjini Ruangwa Aprili
11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wanwake wa Ruangwa baada ya
kuzungumza nao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu mjini Ruangwa
Aprili 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akitembelea soko kuu la mji wa Ruangwa kukagua
hali ya chakula na bei zake Aprili 11, 2016. Alikuwa katika ziara ya
jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa
wa soka wa mkoa wa Lindi , timu ya Namungo FC ya Ruangwa baada ya
kukabidhiwa kombe la ubingwa huo na kuzungumza nao kwenye uwanja wa
michezo wa Ruangwa akiwa katika ziara jimboni kwake , Aprili 11, 2016.
MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa
amefanya ziara katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na
kutoa msaada wa mashuka kwa akinamama waliojifungua.
Pia ametumia fursa hiyo
kuwapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Ruangwa
kutokana na kuwahudumia vizuri wananchi na kuwaomba waendelee kufanya
kazi hiyo kwa mujibu wa maadili ya kazi yao.
Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo
jana wakati alipotembelea wodi ya akinamama waliotoka kujifungua na
kufurahishwa na hali ya utoaji huduma hospitalini hapo, ambapo
aliwasisitiza kuendelea moyo huo kwa sababu wao ndio wamebeba dhamana
ya afya za wananchi.
“Nimefurahi kukuta wazazi
wanahudumiwa vizuri na wenyewe wamekiri kwamba huduma zinazotolewa
hospitalini hapa ni za kuridhisha, tofauti na tulivyozoea kusikia
wagonjwa wakiwalalamikia wauguzi, hivyo ni jambo la kujivunia, hongereni
sana” amesema.
Mmoja wa wagonjwa waliolazwa
katika wodi hiyo Hamisa Rashid ambaye amelazwa katika wodi hiyo amesema
alifikishwa hospitalini hapo wiki mbili zilizopita akiwa katika hali
mbaya na ameweza kuhudumiwa vizuri na sasa anakaribia kutoka.
“Mimi nilikuwa sijitambui, siwezi
kufanya kitu chochote lakini baada ya kuletwa hospitalini hapa madaktari
kwa kushirikiana na wauguzi wamenihudumia vizuri na sasa naweza hata
kwenda chooni mwenyewe na bila msaada wao mimi ningekuwa nimepoteza
maisha kutokana na hali yangu ilivyokuwa,” amesema Hamisa.
Mbali na kutoa msaada huo wa
mashuka pia ametoa baiskeli mbili kwa ajili ya wanawake wawili walemavu
lengo likiwa ni kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii kwa urahisi.
Akizungumza baada ya kupokea
msaada huo, Rehema Omary amemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo,
ambapo alimuomba Waziri Mkuu, Majaliwa awawezeshe kwenda kushiriki
katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na walemavu ikiwemo michezo.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa
Lindi, Godfrey Zambi amewataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi
kwa bidii na kuachana na utendaji kazi wa mazoea kwa sababu umepitwa na
wakati.
Pia amesema amefurahishwa na
kitendo cha wagonjwa kukiri kuwa wanahudumiwa vizuri tofauti na
hospitali zingine hivyo kuwataka kuendelea na ari hiyo ya kufanya kazi
kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment