Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi jezi seti 20 na mipira 20 kwa walimu na manahodha wa shule zote za Sekondari zilizopo wilayani humo jana .shule hizo hivi sasa zipo kwenye maandalizi ya mashindano ya UMISETA Picha na David John
MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi jezi seti20 na mipira 20 zenye thamani ya sh.milioni 4katika shule zote za Sekondari zilizopo katika Jimboni hapa.
Akikabidhi jezi hizo wilayani hapa jana katika hafla
fupi iliyowakutanisha walimu wakuu,wanamichezo,watendaji wa halmashauri
,pamoja na Ofisa Elimu ,Ulega amesema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa
lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia
nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
Amesema kuwa michezo licha ya
kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa
Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
“Ndugu zangu walimu na manahodha
wa timu zote Kutoka shule 20 za sekondari zilizoponda ndani ya Jumbo
langu la Mkuranga nimetoa vifaa hivi ili muweze kushiriki vyema katika
michezo ya shule za Sekondari UMISETA nakutuletea mafanikio,”alisem
Ulega
pia amesema kuwa anatambua kuwa
kuna changamoto za kutosha katika michezo hususani vifaa vya michezo Kwa
kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo huku akiwataka wanafunzi na
walimu hao kusimamia vyema.
Aidha Mbunge Ulega amehaidi kutoa
ushirikiano wa dhati Kwa walimu na viongozi mbalimbali wa halmashauri
hiyo ili Kwa pamoja kuharakisha maendeleo jimboni hapa ikiwamo michezo.
Pia amewaambia viongozi hao
kujenga mashirikiano ya Katibu na yeye kama mwakilishi wao yupo tayari
Kwa wakati wowote kutumika na kusikiliza maoni yao.
Kwaupande wake Ofisa Elimu wa
Halmashauri Kwa upande wa shule za Sekondari Benjamini Majoya
akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa Mbunge Ulega amefanya jambo
ambalo halijawahi kufanywa Kwa viongozi wengine waliotangulia.
Amesema kuwa watamuunga mkono Mbunge huyo Kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika nyanja ya Elimu na michezo Kwa ujumla.
“Kwanza tunashukuru Kwa vifaa
hivi kwani vimekuja katika wakati muhimu ambapo tunakwenda katika
mashindano ya UMISETA na Kwa vifaa hivi ushindi upo,”amesema Majoya
Pia ameongeza kuwa hakuna ubishi
kwamba michezo ni ajira hivyo lazima watahakikisha vijana hao wanafanya
vizuri katika michezo na taaluma pia.
No comments:
Post a Comment