Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Saidi Meck Sadiki (watatu kutoka kulia) na
Mkuu wa Wilaya ya Siha Dk. Charles Mlingwa ( wa kwanza kulia)
wakiwasili katika lango la Londorosi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Katikati ni mwenyeji wao Betrita Loibooki, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa
Kilimanjaro.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro akiwasilisha taarifa fupi ya Hifadhi ya
Kilimanjaro kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki
akiwa katika lango la Londorosi.
Mkuu
wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Charles Ngendo
akionyesha maeneo ya hifadhi kwenye ramani kufafanua taarifa ya Mkuu wa
Hifadhi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki akiongea na watumishi wa hifadhi, wilaya na mkoa katika lango la Londorosi.
Watumishi wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Wilaya ya Siha na Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akiongozwa
na Mhifadhi Imani Kikoti, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipata fursa ya
kutembea kwa miguu kupanda mlima kuelekea uwanda wa Shira.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro na ujumbe wake kutoka mkoani na Wilaya ya Siha
wakipewa maelezo juu ya vivutio na jiolojia ya uwanda wa Shira kutoka
kwa Charles Ngendo, Mhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Picha
ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea Hifadhi ya Taifa
ya Kilimanjaro. Hapa akionekana na msafara wake na viongozi wa hifadhi
ya Kilimanjaro wakiwa uwanda wa Shira (mita 3962).
No comments:
Post a Comment