Waumini wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima wakiwa kwenye foleni kwa
ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya
damu. Shughuli hiyo imefanywa jana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Mshauri wa MN, Erica Ishengoma
akiandika maelezo baada ya kumsikiliza mmoja wa waumini wa kanisa hilo,
huku wengine wakiwa kwenye foleni kabla ya kutoa damu.
Ofisa Uhamasishaji wa uchangiaji
damu salama, Hamisi Kubiga (kulia) na Erica Ishengoma wakiwapatia chupa
maalumu za kuweka damu baada ya kupima uzito.
Wataalamu wa maabara, Peter
Onesmo (kulia) na Anthony (wa pili kulia) wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) wakiendelea kutoa damu baada ya waumini hao kujitokeza
kwa wingi jana katika kanisa hilo lilipo Ubungo jijini Dar es Salaama.
Mtaalamu wa maabara Anthony wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea na shughuli ya utoaji damu jana katika kanisa hilo.
Hawa Hamisi (18) akichangia damu
jana. Hawa amesema kuwa anasikia fahari kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali hiyo.
Mtaalamu wa maabara wa MNH,
Sebastian Magulu akiandaa chupa za damu baada ya waumini wa kanisa hilo
kutoa damu jana tayari kwa kuhifadhiwa na kusafirishwa hadi Hospitalia
ya Taifa ya Muhimbili.
Muumini wa kanisa hilo, Vedasto Aloysi akitolewa damu jana katika kanisa hilo na mtaalamu wa maabara na Peter Onesmo.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Na Neema Mwangomo
Dar es Salaam, Tanzania.
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat
Gwajima wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu jana ili kuokoa maisha ya
wagonjwa wanaohitaji damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Katika shughuli hiyo ya utoaji
damu MNH kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Kanda ya
Mashariki wamefanikiwa kukusanya zaidi ya chupa nyingi za damu.
Akizungumzia shughuli hiyo
Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa MNH, Hamisi Kubiga amesema kwamba
mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kwani kwa siku chupa
zinazotakiwa kukusanywa ni 70 hadi 100 ili kuweza kukidhi mahitaji ya
wagonjwa wanaohitaji damu.
Kubiga amesema kuwa baadhi ya
makundi ambayo yanauhitaji mkubwa wa damu ni kina mama wajawazito,
majeruhi, na wagonjwa wa saratani hivyo amewaomba Watanzania wajitokeze
kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
“Hivi sasa tunaendesha mpango
wa uchangiaji damu, tunashukuru wapo wananchi wamejitokeza lakini bado
tunawaomba wananchi, taasisi kampuni binafsi na umma waje kwa wingi ili
kwa pamoja tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji,” amesema Kubiga.
Shughuli ya utoaji damu inaendelea jumapili ijayo kwenye kanisa hilo la Ufufu na Uzima.
Endapo taasisi, kanisa, shule
na makundi mengine yanataka kuchangia damu. Wawasiliane na Mkuu wa Idara
ya Maabara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa namba 0754 575 981, Mkuu wa Idara ya Maabara namba0713 777 595 na Ofisa Uhamasishaji wa Damu salama wa hospitali hiyo namba 0754 597 165.
No comments:
Post a Comment