Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya
Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na
menejimenti ya TADB.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama) akizungumza
mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha
pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo wakati wa
kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB,
Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo
na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya
TADB.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Katikati) akifuatilia
maelezo yaMkurugenzi Mwendeshaji wa TADB (hayupo pichani) wakati wa
kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati
wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati
wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati
wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Wabunge wa Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imeipongeza Serikali kwa kuanzisha kwa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yenye lengo la Kusaidia
upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini
Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo
cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi
na kupunguza umaskini.
Wakizungumza na viongozi kutoka
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB wakati wa vikao
vya kamati za Bunge vinavyoendelea jijini Dar es Salaam. Wabunge hao
wamesema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa kuwa itachagiza juhudi za
kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.
Dkt. Mary Nagu amesema kuwa licha ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado
ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kuu
ikiwa ni Ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya
maendeleo ya kilimo nchini.
“Kwa kweli tunapongeza kwa
kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi mikopo mingi kutoka
taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za
bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,” alisema Mhe.
Nagu.
Wabunge hao wametoa wito kwa Serikali kuiongezea mtaji Bnki hiyo ili kuongeza kasi ya utendaji kazi wa Benki hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka
alisema kuwa TADB inajihusisha na aina zote za kilimo kwa ule wigo mpana
wa maana ya kilimo, ambao inahusisha mazao, ufugaji, uvuvi, na bidhaa
zitokanazo na misitu. Na kuongeza kuwa katika kusaidia minyororo ya
thamani ya mazao ya kilimo, TADB itakuwa inatoa fedha kwenye hatua mbali
mbali za Uzalishaji na uongezaji wa thamani kama vile Uzalishaji wa
awali; uhifadhi; usindikaji; uchakataji; usafirishaji; na masoko.
“Uanzishwaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Nchini kama taasisi ya maendeleo ya fedha,
kulitokana na Wizara yangu, na baadaye mawazo ya Wadau mbalimbali chini
ya uratibu wa Baraza la Taifa la Biashara kuhusu jinsi Tanzania
inavyoweza kufikia mapinduzi ya kilimo,” aliongeza Dkt. Turuka.
Kwa mujibu wa Dkt. Turuka,
katika maazimio kumi (10) ya Kilimo Kwanza yaliyofikiwa mwaka 2009,
azimio la tatu lilikuwa kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo.
Hivyo uanzishwaji wa benki hii ni muendelezo wa Serikali katika kutimiza
na kutekeleza maazimio ya “KILIMO KWANZA”. Hii ilitokana hasa na
kuwepo kwa changamoto mbali mbali kwenye Sekta ya Kilimo ikiwemo
upatikanaji wa fedha na mikopo ya riba nafuu katika kuendeleza sekta ya
kilimo nchini kwa miradi mikubwa ya kilimo, ya kati na midogo inayolenga
kuimarisha minyororo ya thamani ya Kilimo.
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa
TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kuwa kama yalivyo matarajio ya Serikali,
kuanzishwa na kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Nchini, kunategemewa kuwa na umuhimu wa kusaidia upatikanaji wa mali
ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia
lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda.
Ameongeza pia TADB inatarajia
kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya
usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo pamoja na
kuboresha kwa upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi
ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya
kibiashara kwenye soko.
Benki ya TADB ni mali ya Serikali
kwa Asilimia 100 ya Hisa na kwa kuzingatia muundo wa uendeshaji wa
shughuli za Serikali hususan kwenye masuala ya kifedha, Benki ya
Maendeleo ya Kilimo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Hali
kadhalika, benki iko chini ya Uangalizi wa Msajili wa Hazina kama
yalivyo mashirika mengine ya Umma. Hata hivyo, kiutekelezaji, TADB
inajihusisha moja kwa moja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, kwani
muktadha wa uanzishwaji wake umelenga moja kwa moja kwenye Sekta ya
Kilimo kuliko Sekta nyingine yoyote
No comments:
Post a Comment