Friday, 15 April 2016

WAZIRI WA UCHUKUZI WA UBELGIJI AJIUZULU KWA KUPUUZIA USALAMA WAZIRI WA UCHUKUZI WA UBELGIJI AJIUZULU KWA KUPUUZIA USALAMA.

Waziri wa Uchukuzi wa Ubelgiji amejiuzulu kufuatia tuhuma za kudharau mdororo wa usalama katika uwanja wa ndege wa Brussels kabla ya mashambulizi ya Machi 22.

Vyama vya upinzani vimekuwa vikishinikiza waziri huyo Bi. Jacqueline Galant ajiuzulu.

Wapinzani wamepata nyaraka za siri za Umoja wa Ulaya za mwaka 2015, zilizokosoa hatua za kiusalama katika viwanja vya ndege vya Ubelgiji.

Mashambulizi katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kwenye stesheni ya treni yaliyofanywa na kundi la Dola ya Kiislam yaliuwa watu 32.

No comments: