Thursday, 12 May 2016

Leo katika historia

Marcelo Viera Da Silva Júnior
1988: Marcelo azaliwa

  • Marcelo Viera Da Silva Júnior

MARCELO Viera da Silva Júnior anafahamika zaidi kama Marcelo. Huyu ni msakata kabumbu raia wa Brazil ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Hutumia mguu wa kushoto awapo uwanjani katika nafasi ya ulinzi na winga. Alizaliwa Jijini Rio de Janeiro. Alioa mwaka 2008. Ana mtoto mmoja anayeitwa Enzo Alves Viera. 

Marcelo alianza kusakata kabumbu katika klabu ya Fluminense mwaka 2002 na klabu ya Real Madrid ilimsajili 2007 ambako amecheza mechi 230 hadi sasa akiifungia mabao 15.

Timu ya Taifa ya Brazil aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2006, hadi sasa akifunga mabao 4 katika mechi 39 alizocheza.

                            
  • Katika tarehe hii mwaka wa 1820, Florence Nightingale alizaliwa.
Mwingereza Nightingale ambaye anakubalika kama mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa alizaliwa katika mji wa Floransa nchini Italia.

Nightingale aligundua makosa katika huduma iliyokuwa ikitolewa na wauguzi katika wakati huo na akaazimia kuleta mabadiliko katika huduma ya uuguzi.

Nightingale aliunda shirika la wauguzi kwa nia ya kuleta mabadiliko.

Nightingale alitambulika kama “mwanamke mwenye taa” kutokana na juhudi zake ambazo hazikugundua tofauti ya mchana na usiku alipokuwa akiwatibu wanajeshi waliokuwa wamejeruhiwa. 

Baada ya kuhudumu kama muuguzi katika wakati wa vita Nightingale alirudi mjini London ambapo alifungua chuo cha uuguzi.

Baada ya kifo chake siku yake yake ya kuzaliwa ilitambuliwa kama siku ya wauguzi duniani. 

  • Tarehe hii ya 12 Mei mwaka wa 1927 Ahmet Hikmet Muftuoglu alifariki. 
Muftuoglu alitambulika kwa mchango wake kama mwandishi katika kubuniwa kwa Jamuhuri ya Uturuki na kwa mchango wake katika fasihi ya utamaduni wa kituruki.

Muftuoglu alifuzu kutoka chuo cha Galatasaray na kufanya kazi katika kitengo cha mawasiliano ya nje katika utawala wa Sultani. Muftuoglu alichangia pakubwa katika fani ya uandishi nchini Uturuki kwa kuandika vitabu vingi vinavyoendelea kutumika katika fasihi ya lugha ya kituruki.

  • Katika mwaka wa 1929, tarehe kama ya leo 12 mwezi Mei Uturuki iliadhimisha siku ya Udaktari. 
Uturuki ilianzisha siku ya udaktari katika chuo kikuu cha udaktari cha Haydarpasha.

Chuo kikuu cha kwanza cha Udaktari kwa lugha ya Kituruki Darushifa kiliendelea kuadhimisha siku ya leo kama siku ya madaktari hadi kufikia mwaka wa 1937.

Hapo awali katika enzi za Ottoman siku kuu ya udaktari iliadhimishwa tarehe 14 mwezi Machi.

Kufuatia kuundwa kwa jamuhuri ya Uturuki tarehe 14 iliamuliwa kuwa siku ya maadhimisho ya udaktari.

  • Tarehe hii mwaka wa 2008, China yakumbwa na mtetemeko wa ardhi.
Mtetemeko wa ardhi wenye ukubwa wa 7.8 ulikumba jimbo la Sichuan nchini China.

Watu elfu 70 walipoteza maisha huku wengine laki 4 wakijeruhiwa katika mtetemeko huo wa ardhi.

Mtetemeko huo wa ardhi ulisikika katika miji ya Pekin, Shanghai na katika nchi za India, Pakistan, Vietnam na Thailand.

Huu ulikuwa mtetemeko mkubwa zaidi kushuhudi wa nchini China baada ya tetemeko la Tangshan

No comments: