Baada ya kupondwa sana kwa rapa Desiigner kufanana sauti na Future kwenye wimbo wake wa PANDA ambao ulishika namba moja kwenye chati za billboard producer mkongwe Jermaine Dupri naye alisema kuwa mdundo wa PANDA umeibiwa na kukopiwa moja kwa moja kutoka kwenye mdundo wa Future wa “Fuck Up Some Commas.”
Producer wa Panda kutoka Uingereza Menace amefunguka juu ya tuhuma za kukopi biti nakusema “Timu yangu imesikiliza na kugundua kuwa hakuna chochote kilichofanana kati ya kazi hizi mbili,nimetumia vinanda zaidi na kwenye wimbo wa Future vinanda vichache sana,nimetengeneza biti hii mwaka 2014,nimetengeneza wimbo huu kutokana na style ya Grime kutoka Uingereza”.
Mpaka sasa Menace anasema amewatumia biti wasanii Lil Wayne, French Montana, Ty Dolla $ign, T-Pain na Vado.
No comments:
Post a Comment