Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti
maalum la usalama barabarani Bw. Thobias Msua mmoja wa waendesha
Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni
hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4 na wametoa
msaada huo kwa waendesha bodaboda zaidi ya 4000, makabidhiano hayo
yamefanyika Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akikabidhi koti
maalum la usalama barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu
jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye
thamani ya shilingi milioni 4
Waendesha Bodaboda wakiwa wamejipanga mara baada ya kukabodhiwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vikoti maalum vya usalama
barabarani kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es
salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya
shilingi milioni 4. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa kampuni hiyo Bi. Sophia
Kaihula.
KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imetoa
msaada wa vifaa kusaidia waendesha bodaboda Mtaa Mbezi A, katika
kujiepusha na ajali katika siku ya usalama duniani.
Akizungumza wakati wa kakabidhi
vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Erick Sambu amesema
kuwa vifaa walivyopewa vitasaidia katika kujiepusha na ajali kutokana na
dereva wa gari kuona kifaa hicho.
Amesema kuwa vifaa hivyo vina
thamani ya sh.milioni Nne na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika
makundi mbalimbali kutokana na kazi yao ya kuangalia usalama.
Sambu amesema kuwa SGA katika
kuadhimisha siku ya usalama duniani na kuwataka wadau wengine kuunga
mkono katika kuwangalia watu bodaboda.
Naye Mwakilishi wa Mwanyekiti wa
Serikali ya Mtaa Mbezi A, Carolyne Ngoda amesema kuwa SGA wameokoa
maisha ya vijana wao wanaoshughuli na biashara ya kusafirisa watu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine
No comments:
Post a Comment