WANAFUNZI INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA WATEMBELEA UN TANZANIA.
Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na
Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of
Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki
mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao
walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo
anuai
Mmoja wa wafanyakazi wa UN nchini Tanzania (kulia), akitoa somo kwa
Wanafunzi wa 'International School of Tanganyika-IST' waliotembelea
ofisi hiyo nchini Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali za msingi
zinazofanywa na UN.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International
School of Tanganyika-IST) wakijibu maswali mara baada ya kuelezwa namna
ofisi ya Umoja wa Mataifa, UN zinavyo pambana kutetea haki mbalimbali za
msingi kwa watoto.Baadhi
ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School
of Tanganyika-IST) wakifuatilia maelezo toka UN ya namna ofisi hizo za
Umoja wa Mataifa zinavyofanya kazi hasa kutetea haki mbalimbali za
msingi kwa watoto. Nyuma ni baadhi ya walimu wa IST walioambatana na
wanafunzi hao
No comments:
Post a Comment