Thursday, 28 April 2016

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Butusyo Mwambelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya  (Hawapo pichani)katika kuzngumzia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu katika duka la kuuzia  vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .

Baadhi ya askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.


Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya)
JESHI  la Polisi mkoani Mbeya  limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watu watano  wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine , walifika kijijini hapo  kwa lengo la kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji  mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la Matundasi Chunya..
Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha mochwari katika  hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na makazi yao bado hayajajulikana.
Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio  watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo  kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS   aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo .
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza  kurusha  risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka .
Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha msako usiku huo   na kufanikiwa kuwaua majambazi  wengine wawili  ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu hao.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana
bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27  kwenye magazine.  Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja na panga .
Mwambelo  alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao bado hayajatambulika.

No comments: