Thursday, 28 April 2016

Timu za mpira wa pete na miguu za Bunge zapongezwa kwa kufanya vizuri mashindano ya Muungano.

AK1 
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
AK3 
Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
AK4 
Wabunge wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
AK5 
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa Bunge leo mjini Dodoma.
AK6 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake waliomtembelea leo Bungeni, mjini Dodoma.
AK8 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Bungeni, mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kushiriki vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kurudi salama mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi hizo za Spika zimetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kwa niaba ya Spika alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge hadi jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene  na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.
Timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni timu za mpira wa miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa kuishinda timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15 wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1
Kushiriki kwa Wabunge katika mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo kati ya pande mbili za Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya zao.
Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi mbalimbali katika kujenga na kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani mwema.
Ushiriki wa Wabunge kwenye mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki michezo mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi mazoezi ya viungo (Gym).

No comments: