Thursday, 28 April 2016

Nape Apania Kuiboresha Tasnia ya Habari.

index 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.

Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.
 
Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.
 
Kwa jinsi hii tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Nchi kwa kutujalia kupata kiongozi wa nchi ambaye ni mchapakazi na aliyejaliwa kipawa cha kuona mbali kwa kuwaweka viongozi wa chini yake katika nafasi za uongozi wanazostahili.
 
Sekta ya habari ni sekta nyeti na muhimu sana katika dunia hii kwa kua bila kupashana habari na kujua kinachoendelea daima hakutakua na maendeleo kwa hiyo, ni sekta inayohitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuhakikisha kwamba inachukuliwa uzito na inapewa kipaumbele kwa kupewa vifaa na elimu ya kutosha ili kuepusha upotoshaji na kukosekana kwa habari muhimu hasa za Serikali zinazotakiwa kuwafikia wananchi kwa muda husika.
 
Tukiangalia katika sekta ya habari, Mhe.Rais hakukosea kabisa kumuweka Waziri Mhe. Nape kwa kuwa ameanza kuitumikia Wizara kwa kasi nzuri na ameonyesha nia ya kuiboresha Wizara hasa kwa tasnia ya habari kwa kuanzia kwenye wizara yake hadi katika ofisi za umma zilizoko mikoani ili kuhakikisha wanahabari wote nchini wanatambua thamani ya kazi yao.
 
Kwa maneno yake aliyoyatoa Jijini Mbeya alipokua akigawa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya mawasiliano yaani ipad kwa maafisa mawasiliano wa mkoa huo alikaririwa akisema,”Nataka Wizara ihamie mikoani” hii haimaanishi kuwa Wizara ihamie mikoani kama alivyosema bali alimaanisha kiutendaji zaidi kuwa yale yote anayoyafanya katika Wizara yake atahakikisha na maafisa wa mikoani pia wanafanyiwa hivyo ikiwemo kugawiwa vitendea kazi pamoja na mambo mengine.
 
Katika kuhakikisha hilo, kwa upande wa sekta ya habari, Waziri Nape ameanza kwa kugawa ipad  kwa maafisa mawasiliano walioko mikoa ya pembezoni ambao wana upungufu mkubwa wa vitendea kazi na kwa muda mrefu wameshindwa kuifanya kazi yao kwa ufanisi kwa sababu ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi hiyo

No comments: