Thursday, 28 April 2016

MWANZILISHI WA TAASISI YA WANAUME KAZINI MAN AT WORK MAXWELL STANSLAUS AKIZUNGUMZA NA WANAUME WALIOKUTANA JIJINI ARUSHA JANA.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wanaume Kazini maarufu kama Man at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
 
Muasisi wa Taasisi hiyo yenye makao yake jijini Arusha Maxwell Stanslaus amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.

Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.

“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi Wanaume zaidi ya Milioni walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema Maxwell

No comments: