Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na ujumbe
kutoka Mtandao Kijinsia Tanzania (TGNP) walipofika ofsini hapo
kwa ajili ya kutoa shukrani zao.
Mwanaharakati
kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani
fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.
fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel.
Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.
“Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu,tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “ MAMA TUA NDOO YA MAJI KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.
Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.
No comments:
Post a Comment