Wednesday, 27 April 2016

MKUU WA WILAYA IRNGA ASHEREHEKEA MUUNGANO KWA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA KIJIJI CHA MUGABIKE TARAFA YA KALENGA.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa katika Kijiji cha Magubike kata ya Nzihi Tarafa ya Kalenga kusikiliza kero za wana kijiji. 

Katika kusherehekea Sikukuu ya Muungano, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alikwenda Kijiji cha Magubike kata ya Nzihi Tarafa ya Kalenga, kusikiliza kero za wanakijiji. 

Mkutano huo ulifanikiwa kutatua kero nyingi na zingine ikiwa ni suala la bajeti, mfano changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya maji pamoja na ujenzi wa Bwawa kubwa ambalo upembuzi yakinifu tayari, ambapo zinahitajika shilingi bilioni 2.5. 

Mkutano wa leo pia ulisuluhisha ugomvi mkubwa kati ya Mwenyekiti wa kijiji na aliyekuwa Mwenyekiti wa ITCOJE, Bwana Msafiri Pamagila. 

Wanannchi walifurahi sana kwani watu hawa wote ni maarufu pia wana wafuasi wengi. Pia katika mkutano huo alikuwepo mzee maarufu na wa siku nyingi Mzee Nyangalima ambaye alisistiza suala la nidhamu ya kufanya kazi naye, pia alilalmika kunyang'anywa trekta ambalo analipia mkopo kwa muda mrefu, trekta hilo liliamuliwa kipewe chama cha msingi. 

Diwani wa kata Mh Steven Mhapa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa pia Makamu Mwenyekiti wa ALAT alishukuru wananchi kwa utulivu na kukemea majungu na uzushi ambavyo vinahatarisha amani.​
Wananchi wa kijiji cha Magubike kata ya Nzihi Tarafa ya Kalengawakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela
Wananchi wa kijiji cha Magubike kata ya Nzihi Tarafa ya Kalengawakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela

No comments: