Wednesday, 27 April 2016

Lil Kesh athibitisha kutengana na lebel ya Olamide.


Msanii wa lebel ya YBNL ya Olamide Lil Kesh amethibitisha kuwa mkataba wake na YBNL imeisha ila mahusiano yake na lebel hio bado yako powa.

Lil Kesh anasema “Mkataba na YBNL umeisha wiki mbili nyuma, ulikuwa ni mkataba wa album moja, video tatu na bosi wangu amenifanyia video tano, ulikuwa ni mkataba wa miaka miwili tu, YBNL Ni lebel ya kutoa wasanii wanaotoa wasanii wengine ndio maana bado mahusiano yangu na lebel hio yako powa kabisa,”
Mwaka mmoja uliopita Olamide alisema hataki wasanii wajiskie ni watumwa kwenye lebel yake.

No comments: