Mama
Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na
mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari
wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mama
Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye
furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa
na hayati mumewe imetimia.
Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa.PICHA NA IKULU

No comments:
Post a Comment