Kipa Joe Hart ameendelea kuipa matumaini Manchester City kufikia mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuokoa vyema michomo miwili dakika za mwisho katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid uliomalizika kwa sare tasa.
Huku mshambuliaji Cristiano Ronaldo akikosa mechi hiyo kutokana na majeruhi ya kwenye paja, Real Madrid ilionyesha makali kidogo ya kusaka goli mwanzoni hadi katika dakika za mwisho ndipo iliponyesha kutishia.
Katika dakika 20 za mwisho za mchezo huo ndipo Jese alipopiga mpira wa kichwa uliogonga goli la Real Madrid, kabla ya kipa Joe Hart kuzuia kiufundi nafasi za kufunga walizopata Casemiro pamoja na Pepe kutokana na mpira ya kona.
Kipa Joe Hart akizuia shuti la Pepe
Gareth Bale akichanja mbuga kwa kuruka daluga kwenye mchezo huo
Cristiano Ronaldo akifuatilia mchezo huo, ambao pia ulihudhuriwa na Ronaldo de Lima
No comments:
Post a Comment