Bondia Ramadhani Shauli akisani
mkataba wa kuzipiga na Salim Salim kutoka Malawi mei 14 katika uwanja wa
ndani wa Taifa kulia ni kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi |
Kiongozi wa PST Anton Ruta akitia saini mkataba wa bondia Nassibu Ramadhani kushoto |
Bondia Nassibu Ramadhani akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi mbele ya katibu mkuu wa chama cha gumi za kulipwa PST Anton Ruta kulia na kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi |
Katibu wa shilikisho la Masumbwi Tanzania Anton Ruta akimsainisha bondia Fransic Miyeyusho |
Bondia Fransic Miyeyusho ‘Chichi
Mawe’ kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi
siku ya Mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa kulia ni katibu mkuu wa
PST Anton Ruta katikati ni bondia Thomas Mashali Picha na SUPER D BOXING NEWS
MABONDIA wanne ambao wanatamba nchini Tanzania wamepigwa pini na promota wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwanzoa
Baada ya kuwasainisha mikataba
mabondia hao kwa ajili ya kucheza mpambano wa kimataifa utakaofanika
jijini Dar es salaam Mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa
Mabondia hao wenye majina makubwa
na ndio tishio kwa sasa katika tasnia ya mchezo wa masumbwi nchini ni
Thomas Mashali atakayegombania ubingwa wa Dunia na Sajjad Mehrabi kutoka Iran
Bondia huyo aliemchachafya
Francis Cheka alipozipiga nae hapa nchini Aprili 19 mwaka 2014 katika
ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kutoka nae droo sasa anakuja kuzipiga kwa ajili ya ubingwa wa Dunia nchini Tanzania
Mabondia wengine waliotia saini ya kuzipiga siku hiyo ni Ramadhani Hauli atakayezipiga na Salim Salim kutoka Malawi na Nassibu Ramadhani pamoja na Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ watatafutiwa wapinzani kutoka nje ya nchi. Nae katibu wa shirikisho la maswumbwi ya kulipwa PST Anton Ruta aliyekuwa msimamizi kwa upande wa chama amesema
kuwa mpambano huo wa kimataifa kwa mabondia wote ambapo takribani ugeni
wa nchi nne kwa pamoja utakuwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuzipiga
hapa nchini likiwemo pambano moja la ubingwa wa Dunia linalosubiriwa kwa
hamu kubwa sana.
|
No comments:
Post a Comment