‘Niliamua kuongeza VISA ili nibaki
Oman, nikatoa pesa mtu anilipie lakini kumbe hakwenda kulipia… nikakaa
nikawa nadaiwa pesa nyingi maana unachajiwa kwa siku pale unapoongeza
siku bila VISA, nikawa sitoki kwenda nje kutembea najifungia tu ndani
kwa miezi yote, nyumbani watu wakapanic napigiwa simu Mama kalazwa
hospitali sababu yangu…. ila baadae ndio nimekuja kupata pesa nikalipa
faini nikarudi Tanzania’ KUOLEWA NA MUARABU OMAN: ‘Waswahili wanaoishi Oman hawapendani, hawapendi maendeleo ya watu, wana majungu na wakawa wananitafutia ugomvi nigombane nipigane Polisi, kuhusu kuolewa sijaolewa…. naapa sijaolewa, watu waliongea hivyo sababu nilikua na boyfriend ambaye ni Mauarabu, mpaka sasa niko naye… tulikua karibu sana ndio maana watu wakahisi nimeolewa nae‘ |
KUHUSU KUVUTA UNGA: ‘Nimekua
nikiona taarifa kwamba mimi natumia dawa za kulevya, nimesikitika sana
na ilitokea mara ya kwanza nilikua na msanii mwenzangu kwenye show sijui
anatumia hivyo vitu kwahiyo watu wakaona tumeshaungana ila sio kweli,
sijawahi hata kuona, najua dada yangu Ray C katokea huko na
aliyoyapitia’ KUHUSU KUVUTA BANGI: ‘Kweli nilikua navuta bangi ila sasa hivi nimeshaacha baada ya kukalishwa chini na familia hata boss, nilikua navuta bangi kutokea nilipotoa wimbo wangu wa pili, nilivuta sababu ya stress…. kuna kipindi nilikua natafuta hata mtu wa kunitungia nyimbo, show zilikata na marafiki zangu walikimbia wote kipindi hicho nilipoandikwa kwamba navuta dawa za kulevya‘ KUHUSU NYIMBO MPYA: ‘Nitatoa single mpya kwenye wiki mbili hizi, tokea niko Muscat natumiwa msg Rachel tumekumiss karibu…. namshukuru Mungu maana msanii kukaa nje kwa miezi alafu watu wakawa wanakumiss hivyo ni bahati… watu wakae karibu tu naachia single mpya soon. |
No comments:
Post a Comment