KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Wananchi (CUF), imeanza vikao vyake
visiwani Zanzibar chini ya mwenyekiti wake ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad
|
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Maasiliano ya Umma wa CUF Hamad Masoud Hamd
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CUF,
Hamad Masoud Hamad, alisema kikao hicho kitaandaa ajenda kwa ajili ya
Baraza Kuu la Uongozi, ambapo pamoja na mambo mengine itaandaa ajenda
kuhusu mwelekeo wa chama hicho na hali ya kisiasa Zanzibar.
Alisema kikao hicho kilichoanza jana kitakuwa cha siku mbili ambapo
kitafuatiwa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi kitakachokutana kwa siku
mbili kuanzia Aprili 2 hadi 3 mwaka huu.
“Kama unavyojua muda mrefu kama chama hatujakutana kujadili mambo
yaliyotokea, sasa kupitia kikao hiki tutazungumzia zaidi hali ya kisiasa
Zanzibar pamoja na ajenda kwa ajili ya Baraza Kuu la Uongozi” alisema
Hamad.
Alisema hatua ya kutokuwepo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chama hicho hakitayumba na badala yake kitakuwa imara zaidi.
Hamadi alisema licha ya hila na vitimbi vilivyofanywa dhidi yao lakini
bado wanasimamia msimamo wao wa kutoitambua Serikali iliyopo madarakani
kwani haina uhalali kwa mujibu wa sheria.
“Kutokuwepo kwetu Serikalini hakuna maana kuwa CUF itakufa, hilo si
kweli, tumepitia masahibu mengi lakini tumeendelea kuimarika, na hili
lililofanyika halitoweza kutuyumbisha kamwe,” alisema
Pamoja na hali hiyo CUF imewataka wapenzi na wanachama wao kuendelea
kuwa watulivu na kutokubali kuchokozeka na baada ya vikao watatoa tamko
ambalo litakuwa dira ya chama hicho. |
No comments:
Post a Comment