|
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni
ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo
leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo
mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya
kidigitali’ (Digital Payment Services). |
|
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo
leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo
mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya
kidigitali’ (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma
za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi
pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia. |
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja
kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao
‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment
Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku
akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya
leseni.
Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa
kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo
kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa
ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha
jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.
Alisema kampuni hiyo inayoundwa
na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na
teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa
kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya
huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake
nchini Namibia.
Hafla hiyo ya makabidhiano
imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia
Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo
nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo
huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu
kibiashara.
|
Kaimu
Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Fortunata Mdachi (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa
MobiPay, Amos Shiyuka mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally
Simba kukabidhi leseni ya biashara kwa Kampuni ya Agano Safi
itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali’
(Digital Payment Services). |
|
Picha ya
pamoja baina ya viongozi wa pande zote mara baada ya zoezi la
kukabidhiana leseni kukamilika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni
ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi.
Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu
wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa
TCRA, Fortunata Mdachi. |
|
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi
wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa
MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya
Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu
Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi katika picha ya
pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. |
|
Balozi wa
Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla
ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini
Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo. |
|
Balozi wa
Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla
ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert
Mhilu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka (kulia). |
|
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo. |
|
Balozi wa
Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu
Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya
zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. |
No comments:
Post a Comment