Mapumziko ya lili mbalimbali kupisha mechi za kimataifa yamemalizika,
sasa wachezaji wanarejea kwenye vilabu vyao kuendelea na majukumu yao.
Mwishoni mwa juma hili zitapigwa mechi kibao kutoka ligi za mataifa
mbalimbali, lakini akili, macho na masikio ya dunia nzima ni juu ya
mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Madri ‘El Clasico’ mchezo wa ligi ya
Hispani maarufu kama La Liga.
Barcelona wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa mbele ya Madrid kwa
pinti 10 wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, mchezo huo utagubikwa na
hisia juu ya kifo cha gwiji wa Barcelona Johan Cruyff aliyefariki juma
lililopita na Barcelona wamepanga kutoa heshima zao kwa nyota huyo
kwenye mchezo huo dhidi ya Madrid.
Siku hizi game ya El Clasico si vita kati ya Real Madrid dhidi ya
Barcelona pekee bali na fursa kwa watu kuwalinganisha Cristinano Ronaldo
na Lionel Messi ndani ya uwanja kutokana na upinzani wa ubora wa
wachezaji hao nyota wa timu mbili tofauti.
Bila shaka hawa ndiyo wachezaji nyota kuwahikutokea katika vilabu
hivi kuwa na upinzani mkubwa kwa wakati mmoja wakichezea vilabu vyao. Ni
fursa nzuri ya kuwashuhudia Messi na Ronaldo wakicheza katika timu
zenye upinzani mkubwa angalau mara mbili au zadi ndani ya msimu mmoja.
Ukweli ni kwamba, wawili hao wamepokezana tuzo ya Ballon d’Or katika kipindi cha miaka nane mfululizo.
Kuelekea mchezo wa El Clasico, ukilinganisha rekodi ya wachezaji hao
kufunga magoli tangu Ronaldo alipojiunga na Madrid inafanana kwa kiasi
kikubwa sana.
Ronaldo na Messi wanamagoli sawa wakiwa wacheza idadi sawa ya mechi, huku Messi akimzidi Ronaldo kwenye upande wa assists.
El Clasico tangu msimu wa 2009-10…
MESSI
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
10 idadi ya assists alizotoa
CRISTIANO
24 idadi ya mechi alizocheza
15 idadi ya magoli aliyofunga
2 idadi ya assists alizotoa
Gazeti moja la Madrid linalofahamika kwa AS limelinganisha rekodi za
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi juu ya mchezo wa El Clasico, angalia
ukurasa ma mbele wa gazeti hilo hapa chini. |
No comments:
Post a Comment