Kikao
cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kitaendelea kesho Jumamosi saa 3 asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo
Karume, na maamuzi yake yatatangazwa saa 7 mchana.
Kamati inakutana kwa ajili ya
kumalizia shauri la upangaji wa matokeo Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes
League) kundi C inayozihusisha timu za Geita Gold, JKT Kanembwa, JKT
Oljoro na Polisi Tabora.
Viongozi watakaohojiwa na Kamati
ya Nidhamu ni, Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
mkoa wa Tabora), Fateh Remtullah (Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu
mkoa wa Tabaora), viongozi wa benchi la ufundi Polisi Tabora, Mrisho
Selemani, Boniface Komba, Bernard Rabiamu.
Kamati pia itawahoji Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita, Salum Kurunge na mwenyekiti wa
Klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita.
|
No comments:
Post a Comment