Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkururugenzi wa Idara ya Misitu
na nyuki kutoka Maliasili Bi. Gladness Mkamba mapema leo katika
kuadhimisha siku ya upandaji miti iliyofanyika ruvu kaskazini Mkoani
Pwani.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, amewataka
watendaji katika ngazi za uteuzi nchini kushiriki kikamilifu katika
kuhahikisha usalama wa rasilimali za misitu.
Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo
leo katika Pori la Ruvu Kaskazini ikiwa ni siku ya Kitaifa ya kupanda
miti na kueleza kuwa Serikali imekuwa na lengo la kupanda miti milioni
moja nukta tano (milioni 1.5) kwa mwaka mzima katika kila wilaya, na
kuwataka watendaji waliopo katika ngazi za uteuzi yaani Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu wakuu, kuhakikisha lengo hili
linafikiwa na kueleza kuwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili
majina yao yatapelekwa katika mamlaka za uteuzi na kuchukuliwa hatua,
hii ikiwa ni njia ya kupima usalama wa rasilimali hizi.
Akiongea na wananchi katika Pori
la Ruvu Kaskazini, Mh. Mpina alisema kuwa asilimia 61 ya ardhi ya nchi
ipo kwenye hatari ya kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa mazingira
utokanao na ukataji miti ovyo, na takwimu zinaonyesha kuwa takribani
hekta laki tatu nukta sabini na mbili za misitu zinakatwa kila mwaka kwa
matumizi mbali mbali. “mikoa nane nchini iko hatarini kuwa jangwa”.
Alisisitiza.
Akielezea athari, zitokanazo na
uharibifu wa misitu, Mh. Mpina alisema taifa linaweza kutumia mabilioni
ya fedha kwa ajili ya kununua chakula kuwalisha wa Tanzania kutokana na
ukosekanaji wa mvua ,vyanzo vya maji kukauka, upatakinaji wa umeme kuwa
wa kusuasua kutokana na uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji.
Kwa upande Mwingine Mh. Mpina
alisema kuwa serikali imekata miti kwa sababu mbalimbali za msingi ikiwa
ni pamoja ujenzi wa miundo mbinu kama vile barabara, reli ujenzi wa
bomba la gesi, hivyo basi kuna jukumu kubwa la kupanda miti mingi zaidi
ya hiyo iliyokatwa.
Akitolea Mfano wa taasisi za
huduma ya misitu Nchini (TFS) iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na
Utalii, Mh. Mpina aliainisha kuwa taasisi zote za serikali zisaidie
taifa kubainisha ni mazao gani ya misitu yanaweza kupandwa katika
maeneo gani kulingana na mahitaji ili kuweza kunusuru upotevu wa
rasimali ya misitu. |
No comments:
Post a Comment