Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa
kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa nawanamitindo
Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.
Akizungumza
Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango
aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo
lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na
kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.
Jokate
amesema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule
hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata
viwanja vya michezo hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki
michezo kwa urahisi zaidi.
“Pale
Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua
mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama
wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea
uwanja wa Basketball na Netball,” amesema Jokate
Ameongeza
kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye
alikubali kutoa Milioni 10 kupitia Taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo
kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani
kushiriki michezo tofauti na hapo awali.
Aidha
amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika
shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika
kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja
vya michezo katika Shule ya Sekondari Kinyerezi na Shule ya Sekondari
Maposeni iliyopo wilayani Peramiho, Ruvuma.
|
No comments:
Post a Comment