Friday, 1 April 2016

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi atembelea kambi ya wakimbizi nyarugusu mkoani kigoma.

18
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayoshirikiana na Serikali ya Tanzania kutoa huduma katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.

19
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibungho, Anatory Nsamizanala(wa kwanza kushoto), mara baada ya kufika katika shule hiyo inayotoa elimu ya awali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita.

20
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri (wa pili kulia), kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mabamba kilichopo  wilayani Kibondo,mkoani Kigoma.Kituo hicho cha Polisi kinajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR). Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.

21
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Exavery Christopher (aliyevaa kofia nyeupe), akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto), wakati akijibu maswali aliyoulizwa na Naibu Waziri muda mfupi baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji cha Mabamba tayari kwa kusajiliwa kabla ya kupelekwa kambini.Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Ziara iliofanyika tarehe 30/3/2016
 

No comments: