Wizara ya uhamiaji nchini Indonesia
imesema itafanya uchunguzi kubaini iwapo kuna msingi wa kumpiga marufuku
mwigizaji mashuhuri kutoka Marekani Leonard Di Caprio asizuru taifa
hilo.
Hii ni kutokana na ujumbe ambao Di Caprio aliandika kwenye mitandao ya kijamii akiangazia ukataji wa miti.
Wakati
wa ziara yake nchini Indonesia hivi majuzi, mwigizaji huyo alisema
sekta ya kufua mafuta kutoka kwa michikichi inahatarisha mfumo wa
ikolojia wa Leuser.
Latika eneo la Leuser orangutan wa Sumatra, chui wakubwa wenye milia, vifaru na ndovu huishi pamoja porini.
Msemaji
wa waziri wa uhamiaji amesema iwapo ujumbe huo wa Di Caprio
utaorodheshwa kama uchochezi basi atazuiwa kurejea Indonesia. |
No comments:
Post a Comment