KIWANDA cha kutengeneza mbao
cha Fibreboard 2000 limited,cha jijini Arusha, leo kimetoa msaada wa
madawati 1000 yenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa shule za msingi
za mkoa wa Arusha, ambazo zinaupungufu wa madawati hivyo kusababisha
wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu
wa mkoa wa Arusha, mkurugenzi mtendaji wa Fibreboard 2000 limited, Tosk
Hansy, amesema msaada huo ni kuitikia wito wa rais John Magufuli, wa
kuwataka wananchi kuchangia madawati kwenye shule mbalimbali..
Hansy, amesema madawati hayo
ambayo yapo katika hatua ya mwisho kukamilika yatakabidhiwa rasmi juma
tatu kwa uongozi wa mkoa wa Arusha tayari kuyasambaza kwenye shule
mbalimbali zenye upungufu.
Akipokea msaada huo, mkuu wa
mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amempongeza mkurugenzi huyo kwa uzalendo
wake wa kutoa msaada huo na kueleza kuwa tayari halmashauri 4
zilizokuwa na upungufu wa madawati zimejitosheleza .
Amesema kabla ya msaada huo na
mingine kutoka kwa wadau mbalimbali mkoa ulikuwa na upungufu wa
madawati 24,000 lakini sasa tayari mahitaji yaliyobakia ni madawati 6000
tu, ambapo swala la madawati litamalizika kabla ya juni 30 mwaka huu.
Amesema Hansy, amekuwa ni
msaada mkubwa kila mara anapotakiwa kuchangia huwa hana hiana,ameweza
kusaidia milango mipya 20 kwenye hospital ya mkoa wa Arusha ambayo ipo
katika ukarabati ,pia ameendelea kusaidia kwenye ukarabati wa kituo cha
afya cha Ngarenaro, jijini Arusha.
Amesema madawati hayo
yatasambazwa kwenye halmashauri zote kulingana na mahitaji .Kwa upande
wake katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Adoh Mapunda, amesema mkoa wa
Arusha una jumla ya shule za msingi 515 ambazo ni za serikali, na
sekondari za serikali ni 141,
Amesema wilaya zenye upungufu
mkubwa wa madawati ni Karatu na Arusha DC ,hivyo madawatio mengi
yatapelekwa kwenye halmashauri hizo ili kuondoa tatizo la upungufu wa
madawati.Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu
No comments:
Post a Comment