Goli la kwanza lililofungwa na Jamie Vardy katika kipindi cha kwanza liliwafanya wenyeji Leicester City kuongoza, na baadaye Vardy alipewa kadi ya njano ya katika dakika ya 56 kwa kujirushwa kwenye eneo la penati na kulazimika kutolewa nje.
Alikuwa Andy Carroll aliyesawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 84 na kisha baadaye Aaron Cresswell kufunga goli safi katika dakika ya 86, hata hivyo penati ya Ulloa ilifanya mchezo kuisha kwa sare ya mabao 2-2.
Jamie Vardy akipachika bao la kwanza la Leicester City
Jamie Vardy akimbwatukia refa baada ya kumpa kadi ya pili ya njano
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Uingereza hii leo magoli yaliyofungwa Roberto Firmino na Daniel Sturridge yaliiwezesha Liverpool kutoka na ushindi ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth.
Katika mchezo huo iliwalazimu wenyeji Bournemouth kuongojea hadi dakika za mwisho ili kupata goli la kufutia machozi lililowekwa kimiani na Joshua King lililofungwa baada ya dakika ya 90.
Kipa wa Bournemouth akiruka bila ya mafanikio kuuzuia mpira uliotinga wavuni
No comments:
Post a Comment