Idadi hii ni sawa na asilimia 52 ya watu wote wenye simu za mkononi. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, kupitia ripoti yake, imedai kuwa idadi ya watu wenye simu za mkononi imefikia watu 39,808,419.
Mwaka 2014, watumiaji wa simu walikuwa milioni 31.86 na watumiaji wa internet, milioni 11.35.
TCRA imedai kuwa idadi ya watumiaji wa simu na internet imepanda kutokana na kuwepo smartphone za bei chee na kuongezeka kwa miundo mbinu ya mtandao wa 3G.
Hadi sasa asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania yenye watu milioni 47 wanatumia simu za mkononi. Hiyo inafanya kuwepo na fursa nyingi kwa makampuni katika biashara na huduma za internet na simu.
No comments:
Post a Comment